Akaongeza kusema: Hivi sasa tuko katika mwaka wa pili wa Dhoruba ya Al-Aqsa, ambapo idadi ya mashahidi imefikia 41,000, na matokeo yake ni kama ifuatavyo:
Kwanza: Israel haiwezi kuangamiza Muqawamah (Upinzani) wa Gaza. Pili: Kushindwa kwa jamii ya Kimataifa katika kuharibu Muqawamah. Tatu: Kuongezeka kwa mwamko wa Kiislamu na Kimataifa dhidi ya Israel. Nne: Mifarakano na hitilafu ndani ya utawala wa Kizayuni. Tano: Kuondolewa kwa Barakoa (Mask) ya Ulimwengu wa Magharibi na madai yao ya Haki za Binadamu na Uhuru wa Mataifa. Sita: Kuingia kwa Iran, Iraq, Lebanon na Yemen katika mstari wa mbele wa mapambano ya Upinzani (Muqawamah). Saba: Kuongezeka kwa mhimili wa Upinzani (Muqawamah). Nane: Ni kwamba mipigo ya Iran yamethibitisha kuwa Israel ni nyumba ya vioo.
Kuhusu Ayatollah Sistani, Hojjat-ul-Islami wal-Muslimina Qabanchi alisema: Israel ilimlenga Ayatollah Sistani kwa ajili ya kumuua kigaidi, huku ikijua kwamba mtu huyu ni mshika bendera wa amani na ubinadamu.
Imam wa swala ya Ijumaa wa Najaf al-Ashraf ameongeza kuwa: Suala hili linaonyesha kuwa Israel ni kundi la kigaidi, nasi tukiwa tunaendelea na kukilaani kitendo hiki (kitisho cha Israel kwa Ayatollah Sistani), tunauonya utawala dhalimu wa kizayuni juu ya uvamizi wowote dhidi ya Iraq, kwa sababu hilo linaiweka rasmi Iraq katika mstari mbele wa Upinzani (Muqawamah).